Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kasi ya uingizaji wa vitu haramu na biashara ndani ya magereza nchini uliifaya wizara kustushwa na hali hiyo na kuamua kuunda kamati ya uchunguzi upungufu na mianya iliyokuwa ikitumika.
Amesema hivi sasa jambo hilo likijitokeza kwenye gereza lolote, hatua zitaanza kuchukuliwa kuanzia kwa mkuu wa gereza na watumishi wengine watakaokuwa wamehusika au kuzembea kwa namna yoyote ile.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza akiwa na uongozi wa Gereza la Butimba, alisema tayari kamati iliyoundwa imekamilisha kazi yake na kukabidhi wizarani taarifa na mapendekezo yake ya namna ya kuthibiti uingizwaji wa bidhaa haramu gerezani zilizokatazwa.
“Ni kweli hali ya uingizwaji wa bidhaa ndani ya magereza ilitushtua sana kama wizara, ikatubidi kuunda tume ya uchunguzi namna vitu hivyo harama vinavyoingia, lakini nisema mpaka sasa tatizo hilo limepungua na imani yetu litaisha kabisa.
“Angalizo ambalo tumejiwekea ni kwamba ikitokea gereza fulani kumetokea hali hiyo, makamanda na watumishi wengine watawajibika papo hapo, wito wangu ni kuwataka kuwa wakali kweli kweli, haiwezekani sehemu kama ile kukafanyika biashara haramu, kama wizara tumeyapokea mapendekezo hayo na kuyafanyia kazi.
Hata hivyo Masauni alimtaka Mkuu wa Gereza la Butimba, Hamza Rajabu kumweleza anavyotekeleza ilani ya viwanda anavyoitekeleza ambapo alisema ndani ya gereza hilo kuna kiwanda cha ushonaji nguo na wamekuwa na wakipata kazi mbalimbali kutoka kwa mashirika ya umma na binafsi.
Licha ya kupewa majibu hayo lakini Masauni alisema alichogundua uongozi wa gereza hilo bado hauna mpango mkakati wa kuliwezesha gereza hilo kujitegemea kwa chakula licha ya uwepo na ardhi yenye ukubwa hekari 479 za kulima mazao mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mwanza.
Hata hivyo alisema kama mkuu wa gereza la Butimba, wamejipanga kuanza kujenga nyumba za watumishi kwa kutumia wafungwa hao na hadi sasa wameanza ujenzi wa nyumba mbili huku akiiomba Serikali kuwasaidia au kutekeleza maombi wanayofikisha wizarani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.