Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa ufanisi kwenye kutekeleza maagizo mbalimbali ya viongozi na mwenendo mzuri wa Ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha yanayozingatia sheria.
Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo leo jumamosi juni 25, 2022 wilayani Magu wakati wa Baraza la Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa ripoti ya Mwaka 2020/21 ambayo imewapatia Halmshauri hiyo Hati Inayoridhisha.
"Nawapongeza kwa kuwa wasikivu na kutopuuza maagizo ya viongozi, mmeyatendea haki maelekezo na vilevile umakini wenu kwenye kujibu hoja wakati wa ukaguzi na haya ndio matunda leo tumekutana muda mfupi kupeana maelekezo ya kurekebisha dosari kidogo zilizojitojeza." RC Gabriel.
Vilevile, ametoa wito kwa watumishi waliolipwa fedha kinyume cha taratibu kurejesha fedha hizo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na Halmashauri kuhakikisha wanakamilisha Miradi mbalimbali iliyoanzishwa yenye thamani ya zaidi ya Tshs Bilioni 5.
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe Salim Kalli ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa ufanisi kwenye ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha na amewashukuru viongozi wa Halamshauri hiyo kwa ushirikiano na kamati ya Usalama na amewaahidi kuendeleza ushirikiano ili kuwaletea maendeleo wananchi.
"Baada ya baraza hili halmashauri lazima muwe na mpango kazi mzuri wa kufuatilia maagizo yote yaliyotolewa na wakuu wa idara hakikisheni mnashiriki kwa kina kwenye kujibu hoja zote." Mkaguzi wa ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu, Mhe Simon Pandalume amekiri kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa madawati kwenye baadhi ya shule kwenye Halmashauri hiyo na ameahidi kuwa kupitia fedha za mapato ya ndani wanakwenda kulitatua tatizo hilo kwa kushirikisha na wananchi na wadau.
"Mhe Mkuu wa Mkoa, tumeshavuka malengo ya makusanyo kwa 130% ya makusanyo na tumeshapeleka Tshs Bilioni 1 kwenye miradi ya Maendeleo wakati tulikasimia Tshs Milioni 800 na Milioni 260 tumevikopesha vikundi ikiwa tulikasimia kupeleka milioni 200 tu, haya ni matunda ya maelekezo yako na tunakushukuru sana."amebainisha Mwenyekiti.
Awali, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza, Waziri Shabani alisema Mwaka 2020/21 Halmashauri ya Wilaya ya Magu ilifanyiwa Ukaguzi na kupata Hati Inayoridhisha na kwamba kuanzia 2013/14 hadi 2021 Halmashauri hiyo imekua na jumla ya hoja 32 ambazo hazijatekelezwa kikamilifu na hazijafungwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.