Halmashauri zetu zijengewe uwezo ili ziweze kujitegemea kifedha na kimapato : RAS Balandya
Leo Novemba 8,2023 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amefungua mafunzo ya mwongozo wa uanzishwaji na usimamizi wa Kampuni mahsusi za uendeshaji wa miradi ya vitega uchumi kwenye mamlaka za Serikali za mitaa na kushauri Halmashauri ziendelee kujengewa uwezo ili ziweze kujisimamia na kuondokana na kupata ruzuku kutoka Serikali kuu.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara kwenye ukumbi wa mikutano Gold Crest Mtendaji huyo wa Mkoa amebainisha kuws zipo baadhi ya Halmashauri zinakusanya mapato ya zaidi ya Shs bilioni 20 kwa mwaka hivyo zikipatiwa mafunzo namna ya kubuni na kusimamia miradi kwa weledi zitapiga hatua zaidi ya kimapato.
"Pamoja na sera, sheria na miongozo mbalimbali bado mamlaka za Serikali za mitaa zinapata changamoto ya uendeshaji na usimamizi wa miradi ya kiuchumi ikiwemo kuingiliwa kisasa, uzoefu mdogo wa watumishi na mapugufu katika usimamizi wa fedha na kusababisha kutofikiwa kwa malengo ya miradi na vitega uchumi husika," Balandya.
Aidha, ameipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji UNCDF kwa kuona umuhimu wa kuandaa mwongozo wa Kitaifa wa uanzishwaji na usimamizi wa Kampuni mahsusi za kuendesha na kusimamia miradi ya vitega uchumi vya Halmashauri.
"Ndugu mgeni rasmi Ofisi ya Rais,Tamisemi na Wizara ya Fedha pamoja na wenzetu washirika wa maendeleo UNCDF tunatarajia kupata matokeo yenye tija baada ya mafunzo haya ambayo nia yake ni kuhakikisha miradi yote ndani ya Halmashauri zetu hapa nchini inakuwa na tija na hatimaye kuleta maendeleo kwa wananchi wetu,"Johnson Nyangi,Mkurugenzi Ofisi ya Rais,Tamisemi Uratibu wa Mikoa.
Amesema pamoja na hayo Serikali kwa kushirikiana na UNCDF pia imetoa mwongozo wa namna ya kuandaa miradi ya uwekezaji ya kuzalisha mapato lengo likiwa ni kuziwezesha mamlaka za Serikali za mitaa kuandaa maandiko ya miradi itakayokidhi mahitaji ya kupata fedha kutoka vyanzo mbadala ikiwemo benki na hatifungani.
Mafunzo hayo ya siku nne yamewashirikisha wakuu wa Idara za mipango na uchumi kutoka baadhi ya Halmashauri za mikoa ya Mwanza,Tanga,Kigoma na Dodoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.