Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewaagiza maafisa Uhamiaji kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali kwa kutoa huduma stahiki .
Hata hivyo alisema pasipoti za zamani zitaendelea kutumika hadi January 2020 ambayo ndiyo itakuwa mwisho wa matumizi yake hivyo maafisa hao waendelee kutoa huduma stahiki zinazofaa kwa kutoa elimu kwa wananchi ili kuona umuhimu wa vitambulisho hivyo .
Kwa upande wake Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza Paul Eranga alisema katika zoezi hilo wameyafanyia kazi maombi 30,941 hivyo aliwataka wananchi kuchangamkia fursa kwani mfumo huo ni rahisi ambapo mtu anaweza kupata pasipoti kwa muda mfupi.
"Tunaomba Wananchi watoe taarifa mapema pindi watakapokuwa na wasiwasi na mtu kuwa siyo raia ili sisi tuweze kubaini suala hilo ,pia mwishoni mwa mwaka huu tutakuwa tumeshughulikia maombi ya mikoa yote," alisema Eranga.
Naye mkuu wa wilaya ya Nyamagana. Mhe.Dkt. Philis Nyimbi amewataka wananchi kutunza pasipoti hizi ili kuepukana na gharama zisizo za lazima kwani serikali imegharimia zoezi hilo.
" Kuchukua fomu ni sh. 20,000 ukikubaliwa maombi kama unasifa zilizobainishwa na serikali utalipia 130, 000 endapo ukipoteza kwa mara kwanza itakulazimu kulipia sh. 500,000 kwa mara ya pili utalipia 750,000 ,nawaomba mchangamkie fursa hii ili muweze kupata pasipoti na kuweza kusafiri na kutangaza utalii wa nchi," alisema Dkt. Philis.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.