Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewapongeza Viongozi na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando kwa kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi wa kanda ya ziwa ambazo zimekua zikiboreshwa siku hadi siku.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amebainisha hayo mapema leo julai 15, 2022 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma ya Kisasa ya Upasuaji kupitia Matundu Madogo (Minimally Invasive Surgeries) katika Hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando.
Amesema, wananchi wa kanda ya ziwa wapotao takribani milioni 14 hivi sasa wanapata huduma bora na za kisasa kabisa katika hospitali hiyo huku akizitaja huzuma za magonjwa ya Uzazi Na vizazi, njia ya mfumo wa mkojo, ubongo na upasuaji wa jumla na ametoa wito kwao kuendelea kushirikiana na Serikali na wataalamu wengine kila inapohitajika katika kuendelea kuboresha huduma.
Prof Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa nia ya Serikali kuleta huduma za kibingwa nchini tena katika sehemu ni kuwasaidia wananchi kupata huduma hizo ndani ukizingatia wananchi wengi hawana uwezo wa kifedha kwenda kupata matibabu nje ya nchi na kwamba kwa kutumia wataalmu wa ndani kupeana mafunzo haya inasaidia Madaktari kueneza huduma za kibobezi nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt Fabian Masaga ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya MOI kwa kuwasaidia madaktari wa Bugando kwa kuwajengea Uwezo na kufanya hospitali hiyo hivi sasa kufanya upasuaji kwa kutumia matundu madogo ambao ni wa kisasa.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa, mpaka leo hii zaidi ya wagonjwa 18 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo kwa kushirikiana na Madaktari na wauguzi kutoka Muhimbili na MOI na kwamba Idara zaidi ya tano tutakua tunatoa huduma za upasuaji kwa njia ya matundu madogo katika Hospitali yetu. Dkt Fabian Massaga
"Kabla ya huduma hizi ilikua mtu akipata ajali matibabu daktari alihitaji kufungua kidonda ili kufanya matibabu kama kwenye Magoti lakini sasa daktari anaingia kwenye sehemu za ndani za maungio na kuona tatizo kwa ndani na kulitibu kwa haraka na kwa njia salama kabisa. Dkt. Wilson Masanja.
"Upasuaji huu wa kisasa ni mzuri sana na hii teknolojia inamuacha mgonjwa na makovu madogo sana na hiyo inapunguza mtu kupata athari za maambukizi na unaweza ukafanyiwa leo na kesho ukaendelea na kazi zako kama kawaida" Dkt George Kanani
Awali Dkt. Samweli Byabato, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa jumla alitumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi wa kanda ya ziwa kufanya upasuaji wa kisasa kwa kutumia matundu madogo huku akibainisha kuwa kwa upasuaji mathalani wa tumbo kifaa maalumu kuingizwa kutibu na kuondoa uchafu na mgonjwa analala siku chache na akitoka anaendelea na shughuli zake zake za kiuchumi.
"Nashukuru sana Serikali kwani mie nimefanyiwa upasuaji kwa njia hii na sijasikia maumivu sana na nimeendelea na kazi zangu hata kabla ya wiki, huduma hii ni nzuri sana maana hapo nyuma niliambiwa upasuaji ni wa hatari na unakuacha na maumivu makubwa sana." amesema Bi. Asha Bakari mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji kwa njia ya matundu Bugando Hospitali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.