Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mkoani Mwanza imeshauriwa kuanza kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa wa Selimundu kuanzia ngazi ya Shule ili Wananchi waweze kuelimika vya kutosha na kupunguza wingi wa wanaozaliwa na ugonjwa huo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ugonjwa wa Selimundu Ulimwenguni yaliyofanyika katika Hospitali ya Bugando Mkoani humo huku akifafanua kuwa Elimu zaidi unahitajika kutokana na watu wengi kutopima kama wana vinasaba vya ugonjwa huo.
"Unakuta watu wanaamua kufunga ndoa bila kujuana vizuri nani kati yao ana vinasaba vya Selimundu matokeo yake wanakuja kujaliwa watoto wenye tatizo hilo na wakati mwingine kuibuka hali ya mshangao"
Aidha, Ndugu Samike ameikumbusha Jamii kujenga tabia ya kuwajali na kuwapenda watoto wenye tatizo hilo na siyo kuwanyanyapaa.
Aidha amewaasa jamii kuwahi kwenye Vituo vya tiba na kupata ushauri wa kitaalamu wanapogundua wamepata watoto wenye ugonjwa huo badala ya kukimbilia tiba mbadala au dawa zisizokuwa na msaada.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza DktThomas Rutachunzibwa amesema tatizo la ugonjwa huo bado kubwa kwani takwimu zinaonesha asilimia 7 ya Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimetokana na Selimundu.
"Tunaishukuru Serikali kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na ugonjwa huo kwa kuboresha huduma za Maabara pamoja na Vifaa tiba" Dkt Rutachunzibwa.
Ulimwengu huadhimisha siku ya Selimundu kila mwaka Juni 19 ambapo kwa Tanzania hutumia siku hiyo kuelimishana na kuhamasisha Jamii kujenga upendo kwa Watoto wenye ugonjwa wa Selimundu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.