Wakala wa barabara za mijini na Vijijini-TARURA umetakiwa kuimarisha usimamizi wa miradi ya ujenzi wa barabara ili kuwezesha wakandarasi kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Charles F. Kabeho baada ya kufika kwenye mradi wa barabara misungwi mjini mkoani mwanza yenye urefu wa kilometa Tatu.
Ukaguzi wa matengenezo ya barabara hiyo umemwezesha kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Kabeho baada ya kuikagua barabara hiyo na kubaini kuwa imejengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 42 na kutoa ushauri kuwa wataalamu wahakikishe kuwa wanajirishisha kabla ya makabidhiano.
"Imarisheni miradi ya barabara kwani Serikali na wananchi wanaimani kubwa nanyi,"alisema Kabeho.
Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani misungwi mkoani mwanza umepitia miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billioni mbili.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ufunguzi wa mabwawa matano ya kufugia samaki katika kijiji cha Sawenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.