• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Jenerali Mabeho aiaga Kamati ya Usalama Mwanza

Posted on: June 17th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini kwa Utumishi wake Mema kwa wananchi wa Mwanza na amemtakia Afya njema wakati wote hata baada ya Utumishi.

Amebainisha hayo leo Juni 17, 2022 wakati Jenerali Venancy Mabeyo alipofika kushukuru na kuwaaga wananchi wa Mwanza katika kuelekea kustaafu kwake kwa Utumishi ndani ya Jeshi hilo hapo Julai 2022.


"Wananchi wa Mwanza wanakukumbuka sana kwa namna ulivyoshiriki wewe binafsi kwenye Operesheni ya Uokoaji iliyokua na ufanisi mkubwa iliyofanyika baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere tarehe 20 Septemba 2018 katika kata ya Bwisya Kisiwani Ukara-Ukerewe Mkoani Mwanza". amesema Mkuu wa Mkoa.

"Ndugu Mkuu wa Majeshi, Wana Mwanza  tumeridhika na tunashukuru kwa utumishi wako na tunamuomba mwenyezi Mungu akuangazie mwanga mwingine kwenye maisha yako yote" Mhe Gabriel.

Jenerali Venancy Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama amesema amefika Kanda ya ziwa kuwasalimia na kuwaaga rasmi kwani anafikia mwisho wa Utumishi kwenye Jeshi alilojiunga tangu 1979.

"Kwangu ni faraja kubwa kwamba nimeishi katika nafasi na maeneo mbalimbali, nimejenga familia kama mtumishi ndani ya jeshi na nje ya jeshi na karibu watanzania wote nimeishi nao katika misingi ya kulinda mipaka ya nchi na mali zao." Amebainisha.

"Nafarijika mno kwamba mmenipa nafasi nije niwaage, kanda ya ziwa ndio nyumbani na wengi wangependa wanione na sasa nimekamilisha mzunguko wa Machweo na Mawio na sasa jua linazama kwenye maisha ya kijeshi ambayo nimekaa kwa muda mrefu." Mkuu wa Majeshi.

Aidha, Jenerali Mabeyo amewaasa vyombo vya ulinzi na watumishi kuendelea kushirikiana na ametumia wasaa huo kuwashukuru huku akibainisha kuwa wamemlea na kumuwezesha kufanya kazi kwa utulivu.

"Nitarudi kijijini nilikozaliwa lakini nitakua na fursa za kuzunguka hapa na pale ili nishirikiane na wananchi wenzangu na kwakweli navishukuru sana vyombe vingine vya ulinzi na usalama kwani wamenipa ushirikiano mkubwa sana na ndio maana afya yangu bado ni nzuri kutokana na utulivu na ushirikiano." amesema.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. July 29, 2022
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2022 July 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI ICAP October 21, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Uwekezaji Yashauri Madini yote Yasafishwe Nchini kabla ya kusafirishwa nje

    March 26, 2023
  • Kamati ya Uwekezaji Yaridhishwa utekelezaji mradi wa Daraja la JPM*

    March 25, 2023
  • Mkoa wa Mwanza wachukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa Marburg

    March 24, 2023
  • TAMISEMI ilivyotumia Wiki ya Kitaifa ya Usalama Barabarani Mkoani Mwanza kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii

    March 22, 2023
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 33180, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.