Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema wanapenda kuona Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo linakua kinara katika utoaji wa huduma ili Mikoa mingine ijifunze kutoka kwao.
Mhe. Malima amesema hayo leo Mei 8 2023 kwenye kikao na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF. John Masunga alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoani humo katika kumbi za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Sisi tunatarajia kuwa na uwanja mkubwa na wa kisasa wa ndege hivyo ni matarajio yetu kuwa na huduma bora za kisasa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili na Mikoa mingine itoke ije ikujifunza kwetu," Amesema Mhe. Malina
Pia Mhe. Malima amemkaribisha Mkuu huyo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji siku atakazokuwa Mwanza atembelee baadhi ya visiwa Ziwani Victoria vilivyo na shughuli za kijamii lakini hazina huduma hiyo, hivyo kuwa katika mazingira hatarishi endapo litatokea janga la moto.
"Kuna kisiwa cha Ghana hicho kina kila aina ya starehe na wingi wa watu,lakini ikitokea bahati mbaya janga la moto uwezekano wa kuteketea watu na mali zao ni mkubwa,hivyo naamini ukipata wasaa huo utaona namna ya kuja na jibu chanya"Mkuu wa Mkoa.
Aidha CGF. John Masunga amemuahidi Mkuu wa Mkoa Kumletea gari la kisasa la kutoa hiduma hiyo na uwepo wa kikosi maalumu cha uokoji majini ambacho kwa sasa kipo katika mafunzo.
" Tukuhakikishie kwamba jeshi la polisi la Mkoa wa Mwanza linafanya kazi kwa ushirikiano na jeshi la zimamoto na uokoaji kuhakikisha kwamba tunalinda maisha ya watu,"Amesema RPC. Mutafungwa
Kikao hicho kimewahusisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Naibu waziri wa Madini kama mgeni mwalikwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.