JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAUDHIBITI MOTO ULIOIBUKA JIJINI MWANZA
Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Mwanza limefanikiwa kudhibiti moto uliozuka kwenye sehemu ya juu ya jengo la ghorofa moja la biashara lililoko mtaa wa Karuta Jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya kufika kwenye eneo la tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi ameviagiza vyombo vinavyohusika na majanga na uokozi Mkoa huo kuchunguza na kubaini chanzo cha moto huo mara moja ili hatua zaidi zichukuliwe.
Mhe Makilagi ametoa rai kwa wafanyabiashara mkoani humo kuhakikisha wanasajiri biashara zao kwenye Bima ili kuwa na usalama wa mali zao panapotokea majanga kama hayo.
Aidha, amelitaka jeshi la zimamoto kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kubaini kwa namna gani wanaweza kujilinda na majanga ya moto pindi yanapotokea.
Naye, Mkuu wa jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo lilifika kwenye eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa mali za wafanyabiashara katika eneo hilo.
Halikadhalika, Kaimu Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani humo Kamila Labani amesema wamefanikiwa kuuzima moto huo ili usilete madhara katika majengo mengine yaliyokuwa karibu na jengo hilo huku wakiendelea kuchunguza chanzo cha kuzuka kwa moto huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.