Halmashauri ya Jiji la Mwanza wilayani Nyamagana wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima vyumba vya madarasa 196 yaliyojengwa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 kwa thamani ya Shilingi Bilioni 3.92.
Akizungumza kwenye hafla ya mapokezi ya vyumba hivyo iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Igelegele Mkuu wa Mkoa ametumia wasaa huo kumshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuwajali wananchi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla kupitia Miradi ya Ujenzi wa Miundombinu kwenye sekta ya Elimu.
Mhe. Malima amewapongeza viongozi wa Halmashauri na Wilaya kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na maamuzi ya kujenga Madarasa katika mfumo wa ghorofa kwani inasaidia kutumia ardhi vizuri Wananchi wanaongezeka hivyo matumizi ya ardhi yanazidi kukua.
Amewasihi wazazi, walezi, walimu na wadau wote wa sekta hiyo kuhakikisha watoto wanapata elimu bora waliyoandaliwa kwa kuwajengea Miundombinu hivyo wanafunzi wanapaswa kuongeza kiwango cha ufaulu na ametoa wito kwa wanafunzi hasa wa kike kujibidiisha kwenye elimu na wazingatie kusoma masomo ya Sayansi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwaondolea upungufu wa vyumba vya madarasa uliyokuwepo siku za nyuma kwa kuwaletea fedha za Ujenzi wa Madarasa 196 kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto shule.
"Ni ukweli usiopingika, Mhe. Rais anatupenda sana maana ni mwaka jana tu ametuletea zaidi ya Bilioni 2 kujenga Madarasa hatujakaa sawa ametuletea tena zaidi ya Bilioni 3 na kufanya tupunguze msongamano wa wanafunzi darasani kwani tumeondoa upungufu tuliokua nao wa Madarasa 400 na sasa tatizo hilo halipo." Mhe. Makilagi.
Mapema asubuhi, Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 6 yanayojengwa kwa Mfumo wa ghorofa kwenye shule ya Sekondari Mkuyuni kata ya Mahina na amewapongeza walimu na Viongozi wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa Madarasa ya kisasa.
"Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu tunamshukuru Mhe . Rais kwa kutuletea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa na Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri kwa usimamizi mzuri na nawasihi wanafunzi wenzangu tuyatunze Madarasa haya yaweze kutusaidia." Semfroza Baraka, Mwanafunzi wa kidato cha nne Igelegele.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.