Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wameshauriwa kuwa karibu na shughuli za mahakama ili kuhakikisha ikitenda haki pasipo kumuonea mwananchi huku wakitakiwa kutengeneza mfumo wa masikilizano na kutoingilia mfumo wa kisheria ili kuleta utulivu na ushamilishaji utendaji haki.
Akizungumza katika kikao kazi cha pamoja kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya ,Makatibu Tawala wa Wilaya pamoja na Watendaji wa Mahakama, kujadili muundo na utendaji kazi wa kamati za maadili za mahakimu wa mikoa na wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alisema ofisi ya Mkuu wa wilaya haikatazwi kutengeneza mifumo ya mawasiliano na siyo kuingilia mifumo ya kisheria lakini mifumo ambayo italeta utulivu itashamilisha utoaji wa haki bila kuathiri nafasi ya kila muimili.
Aliongeza kuwa mahakama nayo itahitaji mifumo mingine kwenye utekelezaji wa maelekezo yake hivyo cha msingi ni kuaminiana ili watu wote watambue na kuamini kile kinachofanywa na mahakama kuwa ni haki.
kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Joachim Tiganga ameagiza mahakimu kufanya kazi kwa uzalendo na uadilifu bila kwenda kinyume na taratibu za kisheria na maadili ya kazi ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu kwa uharaka na usawa.
Alisema kila hakimu ni kiongozi kwa mujibu wa sheria hivyo jukumu lake ni kuhakikisha watu wote wanaofanya kazi chini yake na kutekeleza maadili kama ambavyo sheria inavyowataka.
“Ikitokea mtumishi yoyote anayefanya kinyume na maadili na asichukue hatua anachukuliwa na yeye kuwa amekubaliana na uovu uliofanyika na yeye anaweza kuchukuliwa hatua kama kosa la kimaadili”alisema Mhe. Tiganga.
“Maamuzi ya hakimu yamejengwa juu ya imani pindi ambapo imani yake imeondoka kwake anajukumu la kujiondoa kwenye kesi au shauli lililopo mbele yake”aliongeza.
Akizumgumza kwa niaba ya wenzake Mkuu wa wilaya ya Magu Mhe. Dkt.Philemon Sengati alisema watahakikisha wanayafanyia kazi maagizo yote waliopatiwa kwa weledi zaidi na kuhakikisha watumishi wa mahakama wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria taratibu na maadili ya utumishi wa umma .
“Sisi kama viongozi na wenyevita wa hizo kamati tuta hakikisha baada ya hii semina tunakwenda kuwahamasisha watumishi wetu kufanya kazi kwa nidhamu na weredi mkubwa katika kuwatendea haki wananchi”alisema Dkt.Sengati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.