Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amemtaka Mhandisi Mshauri wa mradi wa tenki la maji la unaogharimu billion 6 Buswelu Andrew Mwakagenda kujitafakari baada ya kuongopa wanafanya kazi hadi siku ya jumapili.
Kauli hiyo ameitoa alipotembelea mradi huo na kusema hakuna Kazi inayofanyika jumapili bali kawaleta wafanyakazi ili kuonyesha wanafanya kazi wakati hakuna wanachofanya .
" Hapa hakuna Kazi mnayoifanya kelele ni nyingi sana Mwanza serikali inaleta fedha nyingi ilu kukamilisha miradi itakayo wanufaisha wananchi kazi ifanyike kama hauwezi utatupisha tunapokuja kukagua mradi msituuzie mbuzi kwenye gunia kwa kutuonyesha mnafanya kazi kumbe amna mnachofanya tukiondoka na nyie mnaondoka " alieleza Aweso.
Pia aliiagiza MWAUWASA na RUWASA Mwanza washirikiabe kuhakikisha wanakamilisha mradi wa Igongwe na Kahama kwa wakati ili wananchi wapate maji ,pia kwa washauri wote wa miradi aliwataka kuacha maigizo bali wafanye kazi kwa bidii na kukamilisha miradi yote kwa wakati na watakaposhindwa kujipanga watasaidiwa.
Alisema adhima ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanapata maji safi na salama hiyo ndio Kiu yake hivyo wakandarasi wote watambue hakuna muda wa nyongeza waache janjajanja bali wachape kazi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele alisema katika mradi wa Buswelu ambao utagharimu Billion 6 unatarajiwa kukamilika mwezi October mwaka huu huku kazi zilizopangwa kufanyika zikiwa ni kulanza bomba la Plastic na chuma kutoka kituo cha kusukuma maji kiseke hadi tanki la Buswelu kilimita 9.51 ambapo wananchi zaidi ya 100,000 watanufaika .
Alisema uzalishaji wa Maji Jijini hapa kupitia mtambo wa kapripoint wanazalisha wastani wa lita million 90 kwa siku huku mahitaji halisi yakiwa ni lita million 150 kwa siku hivyo bado wanakabiliwa na upungufu wa takriban lita million 60 kwa siku
" Ili kuweza kutatua ilo tatizo la upungufu wa lita million 60 serikali inatekeleza ujenzi wa chanzo kingine kipya kilichopo eneo la Butimba Magereza." Alieleza Msenyele.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba alisema Wizara itafatilia utekelezaji kwa ukaribu kwani lengo lao kubwa ni miradi ikamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema Mwanza inakabiliwa na changamoto ya maji hiyo inatokana na maendeleo kwenda kwa kasi kubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.