KASI YA UPANDAJI MITI NCHINI IONGEZEKE ILI KUNUSURU UHARIBIFU WA MAZINGIRA: NAIBU WAZIRI MAZINGIRA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza leo Mei 2, 2024 amezindua kongamano la uhamasishaji wa utunzaji wa mazingira lililofanyika kwenye Hotel ya Adden na kuhimiza kasi ya utunzaji wa mazingira iongezeke maeneo yote hapa nchini.
Akizungumza na washiriki wa kongamano hilo lililopewa jina la Jukwaa la Uwakili lililoandaliwa na Taasisi ya DanMission chini ya Kanisa la KKKT, Naibu Waziri huyo amebainisha bado kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira nchini licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
"Nakupongeza sana Askofu Dr. Alex Malasusa kwa kuanzisha mpango huu,ni dhahiri umeonesha kwa vitendo jitihada za Rais Samia za ulindaji na utunzaji mazingira," Naibu Waziri.
Amesema wananchi sasa ni lazima waelimishwe utumiaji wa nishati mbadala badala ya mkaa au kuni na faida za utunzaji mazingira na vyanzo vya maji
Akitoa taarifa fupi ya Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Said Mtanda amesema mkakati wa kuhakikisha mkoa huo unakuwa wa kijani unaendelea kwa upandaji miti kwa wingi na utoaji wa elimu kwa wananchi.
"Mhe.Naibu Waziri hadi sasa Mkoa wa Mwanza umepanda miti zaidi ya milioni 7 na tunaendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji",Mkuu wa Mkoa
Askofu wa Kanisa la Kilutheri KKKT Dr.Alex Malasusa amesema Taasisi ya DanMission inafanya shughuli hizo nchi nzima ikiwashirikisha pia viongozi wa dini ambao wanaoongoza kundi kubwa la waumini.
Wakati huo huo Mhe Mtanda leo amekutana na kufanya mazungumzo mafupi Ofisini kwake na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mhe.Prof.Adilous Kilangi,mazungumzo hayo yamehimiza kushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo na utamaduni.
"Mhe.Balozi tunatambua Taifa la Brazil lilivyopiga hatua katika soka,mkakati wetu ni timu yetu ya Pamba Jiji FC iende huko kufanya maandalizi ya ligi kuu msimu ujao na ututafutie timu bora ya kujipima nayo ubavu," Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.