Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike akishirikiana na Makatibu Tawala wasaidizi Mkoa leo Novemba 2, wametembelea Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukagua miradi Mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Afya, Maji na Miundombinu.
Akiwa Kata ya Buhongwa Samike amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Bulale na kuwataka viongozi wa Kituo hicho kuhakikisha eneo lile linaongezwa na kupanga mipangilio ya majengo kabla ya ujenzi ili kuzingatia utunzaji wa mazingira.
"Mpangilio wa majengo kabla ya ujenzi ni muhimu sana siyo unapanda miti leo kutunza mazingira, kabla haijakuwa unang'oa ili kuanza ujenzi.
Aidha, amewataka TARURA kuhakikisha ile barabara inayoelekea Kituo cha Afya cha Bulale inatengenezwa ili mazingira yawe rahisi kwa wananchi na wagonjwa wanaofika kituo hicho cha afya.
Baada ya kuondoka Bulale Samike amekagua bweni la wanafunzi wenye ulemavu Shule ya Msingi Buhongwa na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo.
Wakati huo huo, Samike amekagua ujenzi wa mradi wa chanzo cha maji Butimba na kuwataka MWAUWASA kuhakikisha wanawasiliana na Mkoa kila hatua wanapokwama ili kuhakikisha ujenzi unaendelea kwa kazi kubwa.
"Niwatake MWAUWASA wawasiliane na Mkoa ili kuhakikisha ujenzi unaendelea kwa kasi inayotakiwa," alisema Samike.
Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora Samike amekagua ujenzi wa vibanda vya wamachinga eneo la mchafukoga na kukuta ujenzi unaendelea na biashara zinaendelea.
Hata hivyo, Samike amemalizia ziara yake Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuongea na watumishi wa Halmashauri hiyo na kuwataka waendelee kuwatumikia wananchi kwa upendo na uaminifu mkubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.