KATUMIENI MAFUNZO HAYA KUTOA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI KWA WANANCHI: RAS BALANDYA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana mwishoni mwa wiki hii amefunga mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwataka wakatoe huduma bora na kwa wakati kwa wananchi huku wakizingatia Sheria za utumishi wa umma.
Akizungumza na watumishi hao Balandya amesema wakufunzi wamewaelimisha mambo kadhaa yakiwemo muundo wa Serikali na shughuli zake,utunzaji wa kumbukumbu na maadili ya utumishi wa umma,yote hayo yakizingatiwa yataleta tija katika utendaji wa kazi
"Wananchi wapo zaidi ya milioni 61 na sisi watumishi wa umma idadi yetu ni laki sita hivyo mnaona kundi kubwa lenye mategemeo kutoka kwetu, hivyo wajibu wetu ni kuhakikisha tunatoa huduma bora licha ya uchache wetu," amesisitiza mtendaji huyo wa mkoa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala,Daniel Machunda amemshukuru Katibu Tawala kwa kuukubali kutolewa mafunzo hayo ambayo Yana lengo la kuongeza ufanisi wa kazi na pia amewapongeza watumishi hao wapya kwa utulivu na umakini walioonesha kwa muda wote wa mafunzo hayo.
"Hongereni sana kwa kuhitimisha mafunzo haya ya siku tatu, mkufunzi amewapitisha katika maeneo yote muhimu,nawaasa mtangulize nidhamu katika majukumu yenu,Machunda.
Akitoa shukurani kwa Ofisi ya mkuu wa Mkoa kutoa mafunzo hayo,mmoja wa watumishi wapya Raphael Mwinyimvua ambaye ni dereva amesema atahakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia yale yote aliyojifunza.
Jumla ya watumishi wapya 12 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo ni madereva 10,mkadiriaji majengo mmoja na mtunza kumbukumbu mmoja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.