Wakazi wa Kisiwa cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza wametakiwa kufanya maamuzi sahihi na kumchagua kiongozi mwenye uwezo,umakini na mzalendo wa kusimimia rasilimali za nchi na kuwanufaisha huku kituo cha afya Ukara kikipandishwa hadhi na kuwa hospitali ya Wilaya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bwisya kilichopo kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ,Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa anasema ili kuwaondolea gharama za usafiri wa wananchi wa Ukara za kufuata huduma nyingine za afya katika hospitali ya Wilaya hiyo iliopo Nansio.
Anasema kuipandisha hadhi kituo hicho cha afya hivyo huduma nyingine zitaongezeka ikiwemo kuongeza majengo sanjari na kuongeza watoa huduma wakiwemo madaktari bingwa huku hospitali ya Wilaya ya Ukerewe iliopo Nansio ikipandishwata hadhi ya kuwa ya Mkoa, pia alitoa ahadi kwa wananchi hao wa Ukara ya kuwaletea gari 1 la kubeba wagonjwa .
"Nimefika hospitalini hapo ipo vizuri nimesalimiana na wazazi kuna watu wanasema hospitali hii imejengwa kwa damu hiyo inashangaza kwani nyie hamkuona maroli yakisomba mchanga?,matofali yakifyatulia sasa unaposema imejengwa kwa damu unamaanisha nini?" anaeleza Majaliwa.
Pia Majaliwa ameweka mashada kwenye mnara wa makabuli ya watu waliofariki katika ajali ya Mv. Nyerere iliyotokea September 20 mwaka 2018 katika Kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe ambapo watu takribani 227 walipoteza maisha.
Naye Mgombea ubunge Jimbo hilo kwa kupitia CCM Joseph Mkundi alishukuru kwa kituo cha afya kupandishwa hadhi na kuwaomba wananchi wampigie kura Rais Magufuli na wagombea wote wa Ccm kwani chama hicho ndicho kinawapenda na kuwajali wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.