MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPINGA DAWA ZA KULEVYA KITAIFA KUFANYIKA MKOANI MWANZA
Mkuu wa mkoa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 28,2024 ametangaza maadhimisho ya siku ya kupinga dawa za kulevya Kitaifa kufanyika Mkoani Mwanza katika uwanja wa Nyamagana.
Maadhimisho haya yanalenga kupinga matumizi ya dawa za kulevya ili kuondokana na athari zake kuathirika kisaikolojia,kimwili ambapo mtu huyo atashindwa kushiriki katika kujenga uchumi wa Taifa na wakwake mwenyewe
“Wananchi ni lazima kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti dawa za kulevya ni vyema kutembelea mabanda yaliyoandaliwa uwanjani ili kuweza kupata elimu ya kudhibiti dawa hizo ”amesema Mtanda
Naye kamishina Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini Aretas Lyimo amesema tukio hili ni muhimu hususani kwa taarifa za kudhibiti na kupinga dawa za kulevya ambapo wananchi watapatiwa elimu ili kuweza kujidhibiti kutokutumia dawa hizo
Vilevile Juni 29,2024 kutakuwa na kongamano la kuthibiti matumizi ya dawa za kulevya yatakayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ya kupinga na kudhibiti dawa za kulevya ni “Wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.