MAADHIMISHO YA SIKU YA ZIWA VICTORIA KUFANYIKA NOVEMBA MWAKA HUU MKOANI MWANZA
Tanzania itakuwa mwenyeji wa kuandaa maadhimisho ya siku ya Ziwa Victoria ambayo yatafanyika rasmi Novemba 25 -29 mwaka huu mkoani Mwanza.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza mhe. Said Mtanda wakati wa mkutano na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Ofisi ya mkuu wa mkoa,amebainisha kuelekea Maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika yakiwemo makongamano na elimu kuhusiana na rasilimali hiyo.
“Kikao hiki kinalenga kutengeneza mkakati utakaowezesha sherehe hizo kufanyika mwaka huu,asilimia 53 ya mkoa wa Mwanza umezungukwa na ziwa halikadhalika mkoa wa Geita,Mara na Kagera “amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Vilevile amesema lengo kubwa la kuwa na siku ya ziwa Victoria ni wananchi kutambua umuhimu wake ambapo shughuli zao zinategemea ziwa hilo vilevile kuendeleza eneo la bonde la ziwa victoria kwa manufaa ya wananchi na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naye Katibu Mkuu wa Taasisi ya bonde la Ziwa Victoria Dkt. Masinde Bwire amewaomba wadau wa maendeleo na mazingira kushiriki katika maadhimisho hayo.
Kikao kazi hicho kimewahusisha pia Makatibu Tawala wa Mikoa ya kanda ya ziwa, pamoja na viongozi wengine waandamizi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.