MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI KATA MWANZA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA VYANZO VYA MAPATO
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai leo Aprili 29, 2024 amefunga rasmi kikao kazi cha Maafisa Tarafa na Watendaji kata Mkoani Mwanza na kutoa maagizo kadhaa ikiwemo uwajibikaji, Uadilifu, Ubunifu na usimamizi mzuri wa vyanzo vya mapato.
Akizungumza na Maafisa hao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu huyo wa wilaya amebainisha usikivu na uzalendo vyote vikizingatiwa vitaleta tija katika utendaji wa kazi kwenye maeneo yao.
"Nawapongeza sana Tamisemi kwa kuyaleta mafunzo haya,hawa Maafisa wanahudumia kundi kubwa la wananchi na pia miradi mingi imejaa maeneo yao,wanapaswa kuwa siku zote watoa huduma bora,"Ngubiagai
"Mheshimiwa mgeni rasmi mafunzo haya hadi sasa tumeyatoa kwenye Mikoa 18 na tumebakiza Mikoa 8 yote kutoka Bara kazi ambayo tunatarajia kuikamilisha baadaye mwaka huu,"Ibrahimu Minja,Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa,Tamisemi
Jumla ya Maafisa Tarafa 341 na Watendaji kata 2574 wamenufaika na mafunzo hayo yanayotolewa kwa awamu nchi nzima kwa lengo la uboreshaji wa utendaji kazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.