Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko amewasihi maafisa ufuatiliaji na tathmini kusimamia misingi ya kazi kwakua hakuna maendeleo bila kuwa na tathmini.
Amesema hayo leo tarehe 12 Septemba, 2025 kwa niaba ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati akifunga kongamano la nne la Ufuatiliaji, tathmini na kujifunza (MEL) Mkoani Mwanza lililowakutanisha wana taaluma huku waliopewa stadi kwa muktadha wa Afrika.
Mhe. Biteko amelipongeza jukwaa la (MEL) kwa kufikia asilimia 75 ya yale ambayo aliyaagiza katika kongamano la 3 lililofanyika Zanzibar 2023 huku akiwasisitiza wafanye kazi kwa kujiamini na wasijali changamoto zinazotokana na kazi zao za tahmini.
"Nawaomba msijione wanyonge usitafutwe kupendwa unafanya kazi za tathmini sema kweli usiogope kuchukiwa kwakuwa mtakua watu mnaotenda haki kwa kutoonesha uoga". Amesema Mhe. Biteko.
Naye Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya Waziri Mkuu(Sera Bunge na Uratibu) Dkt. James Kilabuko akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) amesema washiriki wa kongamano wameweza kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya maswala ya tathmini na ufatiliaji kwa muda wa siku tatu.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashuku na kuwakaribisha tena waandaji wa kongamano kulirudisha kongamano hilo Mkoani mwanza kwa msimu ujao pamoja na kuwahamasisha kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo.
Mkutano huo umefikia maazimio 12 ikiwa ni pamoja na kuhakikisha jamii zinashirikishwa kwenye tathmini na ufatiliaji kwa afua zote, kukamilisha mfumo wa kielektroniki wa ufatiliaji na tathmini, kurahisisha uandaaji wa sera za taifa na mkutano huo kufanyika kitaifa Dodoma kwa mwaka 2026.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.