MAAMBUKIZI YA UKIMWI MWANZA YAPUNGUA : RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashukuru wahisani kwa kusaidia juhudi za kupunguza maambukizi kwa vifaa na rasilimali watu kwa zaidi ya Bilioni 10 kwa kujenga Maabara ya Kisasa ya Uchunguzi wa Magonjwa hususani virusi vya Ukimwi
Ametoa pongezi na shukrani hizo tarehe 29 Mei, 2024 kwenye hafla ya kukabidhi Maabara ya Upimaji Usugu wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Kanda Bugando.
Ameongeza kuwa misaada mbalimbali imesaidia juhudi za serikali za kupunguza maambukizi nchini hadi kuifanya Mwanza kushuka Maambukizi kutoka asilimia 7.2 mwaka 2017/18 hadi 4.7 kwa sasa hivyo uongozi wa Mkoa unathamini sana.
Ameongeza kuwa, Maabara hiyo itasaidia kupima vimelea na maambukizi na kutoa dira kwa afua mbalimbali za kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI na kwamba mikoa ya kanda ya ziwa wamepata sehemu mahususi kwa tiba na uchunguzi.
Mganga Mkuu wa Mkoa Thomas Rutachunzibwa amesema amebainisha furaha ya sekta ya Afya kwa kushirikiana na wahisani hao kwa dahari ya miaka hususani kwenye utaalamu na minundombinu ya kufubaza maambukizi ya Ukimwi.
Mkurugenzi wa ICAP nchini, Haruka Maruyama ameshukuru uongozi wa Mkoa na Bugando kwa kukubari uwepo wa miundombinu hiyo muhimu kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali kwa Watanzania kwani itasaidia kuboresha huduma hizo kwenye ukanda wa ziwa.
Akimuwakilisha Balozi wa Marekani nchini, Mtendaji wa CDC nchini Dkt. Mahesh Swaminathan amesema wanayo furaha kuwepo nchini kwa miaka 15 na kwamba wamesaidia takribani Shilingi Bilioni 4 kutekeleza mradi huo Bundando Hospitali.
Mkurugenzi wa Buganda Dkt. Fabian Masaga amewashukuru wahisani PEPFAR na CDC kwa kushirikiana na ICAP Global Health kuwaboreshea maabara ya kisasa na rasilimali watu na kusaidia kupunguza matumizi ya nishati ya Umeme na Maji.
Ameongeza kuwa Bugando ina maono ya kukomesha magonja ya kuambukizwa pamoja na yake ya ukanda hivyo msaada wa maabara utasaidia juhudi hizo kwani pamoja na miundombinu wamewajengea uwezo watumishi wa maabara hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.