Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamissi Kigwangala amezindua rasmi maandalizi ya maonesho ya kimataifa y a utalii katika Ukanda wa Maziwa Makuu na jukwaa la uwekezaji katika sekta hiyo,yanayotarajiwa kufanyika juni 19 hadi 21 mwaka huu,katika uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza, ambapo aliwahamasisha wawekezaji wa ndani kutumia jukwaa hilo kama fursa ya kuvitambua na kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini.
Akizungumza wakati akizindua nembo maalum ya maonesho hayo ya kimataifa yaliyofanyika jijini Mwanza yanayotambulika kwa jina la Great Lakes International Tourism Expo(GLITE) yanayolenga kuvitanganza vivutio vya utalii vya maeneo ya maziwa makuu yatakayokuwa yanafanyika kila mwaka ambayo yatahusisha mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Shinyanga,Kagera,Mara,Tabora na Kigoma Dkt.Kigwangala ,alisema ili kuhakikisha fursa ya utaliii inaenea kwa nchi nzima,kupitia maonesho hayo yatatangaza vivutio hivyo na kuwavutia wawekezaji ambapo wanatarajia kuweka mabanda zaidi ya 150 .
Alisema,zaidi ni kutangaza vivutio vilivyopo pamoja na kutangaza fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika mikoa hiyo hatimaye kuwataembeza wageni ambao watakuja kwenye maonesho ili washuhudie kwa macho kile kilichotangazwa na kuwaeleza taratibu za uwekezaji ambao watajitokeza ili waelewe kwenye ukanda huu kuna fursa zipi na taratibu zipoje za kupata maeneo ya kuwekeza.
“Mazao ya utalii ni vitu vingi kwa kiasi kikubwa Tanzania tunasifika kuwa na vivutio vya asilia mbapo hiyo ni bidhaa ya kwanza, ya pili hatujawai sana kutumia maji kama mazao ya utalii, kuanzisha sakta hii ya utalii kwa ukanda huu ya kutumia ziwa Victoria na Tanganyika maana yake tunatoa fursa ya watu kuona nini ni wanaweza wakafanya kupitia maziwa haya,linaweza kuwa zao la pili ambalo linaweza kutusaidia kuleta upekee katika ukanda huu,eneo la tatu ni mila na desturi za watu wa maeneo haya,kabila yaliyopo hapa ni mengi mfano Mkoa wa Mara una zaidi ya makabila 16 ambapo una kuta kijiji kimoja kabila hili kijiji kingine kabila jingine,pia kabila hili la wasukuma,tuna madini ya dhahabu na almasi,”alisema Dkt.Kigwagala.
Aidha alisema,ni jambo la msingi kwa hatua hiyo ya awali kwa ukanda huo kuzitambulisha fursa zilizopo ili zijulikane na kusaidia uelewa wa vivutio ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza na kuandaa miundombinu ya utalii ambapo ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015-2020 inazungumzia suala la kukuza utaliii na ielekeza wizara husika kuongeza watalii kutoka milioni 1 mwaka 2015 hadi milioni 2 mwaka huu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani zenye vivutio zitapenda kuja kutangaza vivutio vyao nchini hapa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini {TBB} Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema bodi hiyo ipo tayari kusimamia,kujitolea na kushughulika ili maonesho hayo ambayo ni ya kwanza na ya aina yake yaweze kufanikiwa na kufanyika kwa ngazi ya kimataifa huku akiwahimiza wakuu wa mikoa hiyo inayohusika katika maonesho hayo kutangaza shughuli hiyo kila mara kuwa itafanyika mkoani Mwanza pamoja na watendaji wasekta hiyo wakijipange katika ufanyaji kazi.
Baadhi ya wakuu wa mikoa itakayoshiriki katika maonesho hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella na Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wamesema wapo tayari kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuibua na kuendeleza fursa za utalii zinazopatikana huku Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga akitumia fursa hiyo kutoa ombi la kupatika naeneo la kudumu kwa ajili ya kufanyia maonesho hayo.
“Sisi kama Mikoa tupo tayari tumejipanga kwa fursa zilizopo katika mikoa yetu,ili kuweza kushiriki katika matayarisho, lakini vilevile kuhamasisha wadau kutoka sekta mbalimbalia mbao ni wadau katika sekta ya utalii kushiriki kama ambavyo inatarajiwa mwisho wasiku kutoa mchango wa kutosha kwa maendeleo ya mikoa yetu,watu wetu na nchi yetu kwa ujumla,”alisema Mhe.Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.