MaDAS na Maafisa Tarafa zingatieni majukumu yenu ila mtoe huduma bora kwa wananchi-RAS
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndg.Balandya Elikana amewakumbusha Makatibu Tawala Wilaya na Maafisa Tarafa Mkoani humo kutumia vyema mafunzo wanayopewa ili kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi kwenye maeneo yao.
Akifungua kikao kazi kwa watumishi hao kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Balandya amebainisha bado zipo changamoto kwa wananchi zikiwemo ufahamu wa sheria za nchi na haki zao hivyo huduma zao sahihi kutoka kwa watumishi hao ndiyo zitatoa ufumbuzi wa hali hiyo.
"Unakuta mwananchi anapoteza mali zake halali kama shamba au nyumba lakini anashindwa wapi pa kuanzia matokeo yake anaishia kudhulumika endapo mtakwenda kusimamia vyema majukumu yenu naimani matatizo kama hayo yatamalizika," amefafanua Mtendaji huyo wa Mkoa.
Aidha, ametumia jukwaa hilo kuwapongeza Makatibu Tawala wapya walioteuliwa hivi karibuni na Mhe Rais na kuwapa rai kuteuliwa huko waje na matokeo chanya kwenye maeneo yao ya kazi.
Mtoa mada kwenye kikao kazi hicho Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Daniel Machunda amesema mafunzo hayo ni ya kawaida kwa watumishi hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na hasa baada ya Mkoa wa Mwanza kuwapata watumishi wapya wa kada hiyo ya Makatibu Tawala.
"Lengo la Serikali siku zote ni kuwaona wananchi wake wanaishi kwa amani, usalama na kutambua haki zao zote za msingi katika maisha yao kila siku, sasa sisi watumishi ndiyo daraja kati ya Serikali kuu na Serikali ngazi ya Tarafa au Wilaya katika kuwatumikia wananchi",Machunda.
"Tunapopatiwa mafunzo kama haya yanatusaidia katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku kwa lengo la kuwapa huduma yenye tija wananchi wetu", Gloria Kaywanga,Afisa Tarafa Inonelwa,Misungwi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.