MADIWANI SIMAMIENI KWA WELEDI HALMASHAURI YA UKEREWE-RC MAKALLA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe.CPA Amos MAKALLA amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Ukerewe kusimamia kwa Weledi majukumu yao yote ikiwemo changamoto ya ufaulu wa wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba yake leo wakati wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali za Juni 30 2021-22,Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amesema wawakilishi hao wa wananchi wanapaswa kutambua wanakuwa chanzo cha kuwapigania maendeleo wananchi wao,hivyo changamoto zote wahakikishe zinapatiwa ufumbuzi.
"Kutokana na Jiographia ya Kisiwa cha Ukerewe na asili ya shughuli za kujipatia kipato baadhi ya wazazi hawana muda wa malezi bora ya watoto wao,hali ambayo imechangia ufaulu hafifu",amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Aidha ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Madiwani hao kupunguza hoja za CAG kutoka 19 hadi kubaki 8.
"Tujitahidi kutokuwa na hoja nyingi na badala yake tufanye kazi kwa bidii kwa kufuatwa miongozo na kuepuka uzembe ambao kwa kiasi kikubwa unachangia kuwepo na hoja hizo",Balandya.
Mbunge wa Jimbo la Ukerewe,Mhe.Josephat Mkundi ameshauri kuwepo na mkazo wa elimu kwa wananchi hasa kutokana na aina ya malezi yasiyo na tija kwa watoto wao.
"Ndugu Mwenyekiti wa kikao hiki changamoto nyingine ni uhaba wa chakula shuleni hii nayo ipewe kipaumbele ili wanafunzi watulie na kusoma vizuri",Mhe.Mkundi.
"Mwenyekiti wa kikao tunashukuru kwa maelekezo yako na kuahidi kuyafanyia kazi,tuna ushirikiano mzuri na Waheshimiwa Madiwani katika kuwaletea maendeleo wananchi",Emnanuel Shelembi,Mkurugenzi H/ya Ukerewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.