MAFUNZO YA SPV YASAIDIE HALMASHAURI KUWA NA MIRADI YENYE TIJA : RAS MWANZA
Washiriki wa mafunzo ya mwongozo wa uanzishaji na usimamizi wa kampuni mahsusi ya uendeshaji wa miradi ya vitega uchumi kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa yaani Special Purpose Vihicle (SPV) wametakiwa kubuni miradi itakayoipatia mapato halmashauri ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Oktoba 29, 2024 wakati akifungua mafunzo kwa makatibu tawala wasaidizi mipango na uratibu na wakuu wa Idara za mipango na fedha kutoka Mamlaka za Serikali za mitaa.
Aidha, ameishukuru TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo UNCDF kwa kuja na mpango huo ambao unatoa fursa ya kujadiliana kwa pamoja changamoto na mipango ya kufanya lengo likiwa Halmashauri ziwe na miradi yenye tija na kujisimamia zenyewe.
"Ndugu washiriki wa mafunzo ni imani yangu kutakuwa na tofauti mlivyokuja na mtakavyoondoka nikiwa namaanisha mageuzi mtakayokwenda kufanya kwenye maeneo yenu", Balandya
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya mitaji (UNCDF) Bi. Stella Lyatuu amebainisha kuwa washiriki watafundishwa jinsi ya kuanzisha miradi ya inayoendana na uanzishwaji wa miradi ya kampuni, muundo wa utawala na menejimenti, usajili wa kampuni, vyanzo vya fedha na usimamizi wake.
Washiriki hao wanatoka kwenye mikoa saba ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, na Geita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.