Novemba 14, kila Mwaka Nchini hufanyika Maadhimisho ya Siku ya kupambana na magojwa yasiyoambukiza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb) baada ya kuzindua 2019 na kutangaza rasmi kuwa wiki ya pili ya mwezi novemba 14 kila mwaka yatakuwa yakifanyika ambapo Kimkoa yamefanyika Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Kwanza.
Akizungumza katika viwanja vya CCM Kirumba ambapo maadhimisho hayo yanafanyika mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel amesema magojwa hayo yamekuwa tishio kwa taifa letu hivyo Mkoa unaungana na Mikoa mingine kwa kutoa huduma mbalimbali katika vituo vya tiba.
"Katika kipindi kisichozidi miaka 8 kumekuwa na magojwa yasiyoambukiza kama vile pumu, magojwa ya afya ya akili na yanayotokana na ajali," alisema Mhandisi Gabriel.
"Kwa kila watu 100 wenye umri wa miaka 25 na zaidi 9% wanakisukari 26% wana shinikizo la juu la damu,34% wana uzito uliopindukia na 25% wana mafuta yaliyozidi kwenye damu,hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012(step Survey) alisema
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala amewashukuru wananchi na klabu zote zilizoshiriki katika mbio za wote walioshiriki katika maandalizi ya kuhitimisha siku hiyo.
"Tunafanya mazoezi kwa mwezi mara moja ambapo tunaunganisha club zote na kukimbia km 8 ili kukabiliana na magonjwa ambayo tunaadhimisha mapambano yake leo na nitoe wito kila mmoja aliyefika hapa leo aende akapime magonjwa hayo kwenye mabanda yaliyopo hapa," alisema Mhe.Kasala.
Naye Dkt.Silas Wambura kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi ambao afya zao ni imara wachukulie mazoezi kama sehemu yao ya maisha ili kuepuka na magojwa hayo na wasisahau upimaji wa kike siku wa Afya zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.