Zaidi ya Sh30 billion zinakusanywa kwa mwaka na makampuni 18 ya bima kwenye mikoa saba ya kanda ya Ziwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa (Tira)Sharif Hamad aliyemuwakilisha Kamishna wa Bima Dkt. Mussa Juma kwenye maadhimisho ya siku ya Bima Kanda ya Ziwa, ambapo aliitaja Mikoa hiyo ni Mkoa wa Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kigoma na Kagera.
Alisema, kwa kanda ya ziwa wana madalali 8 na mawakala 75 ambao wanatoa huduma na kuhakikisha bima zinapatikana kwa wananchi mijini na vijijini.
“Katika kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za bima, tumeanzisha ofisi ya msuluhishi wa migogoro ya bima ambayo kazi yake ni kutatua migogoro ya baina ya makampuni na wateja wa bima, badala ya wateja kuyafikisha malalamiko yao mahakamani tukaona kuna haja ya kuanzisha ofisi hiyo”alisema Hamad
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana dk Philis Nyimbi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyataka makampuni hayo kulipa fidia kwa wateja waliopata majanga kwa wakati na sio kuwazungusha.
Alisema wilayani Nyamagana kulitokea majanga ya moto Soko la Mlango mmoja, Buhongwa na kituo cha mafuta cha Moil ambayo yanafundisha mwananchi kukata bima kuna punguza makali pale majanga ya namna hiyo yanapotokea.
Mmoja wa washiriki wa maadhimisho hayo ambaye ni Meneja wa kampuni ya bima ya Britam Kanda ya Ziwa, Said Kadabi alisema kutokana na mfumo mpya wa kuhifadhi taarifa za bima kwa njia za kielektronik (Tira Mis) askari wa usalama barabarani wasiwe wakali kupitiliza pale wanapofanya ukaguzi kwenye magari mfumo ukiwambia bima ni yakugushi kwakuwa mfumo bado haujakaa sawa bali .
“Tumeshatoa malalamiko yetu kwa Tira yanafanyiwa kazi, niwasihi jeshi la polisi liweze kuliangalia hilo na serikali iandae makongamano ili kuwafahamisha watu umuhimu wa bima”alisema Kadab.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.