Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.Philip Mpango amewataka wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Fukwe zilizopo nchini ili kukuza Utalii na Uchumi kwa ujumla.
Akifungua leo Kongamano la kudhibiti Fukwe linalofanyika Mkoani Mwanza,Mhe Mpango amesema nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na Bahari,Maziwa na Mito yenye Fukwe nzuri ambazo zinahitaji uwekezaji wa kisasa utakaochangia pato la Taifa.
"Nina Imani Jukwaa hili la kongamano litakuja na majibu chanya yenye tija kwa Taifa letu kwani nimesikiliza taarifa za utangulizi za kitaalamu zinazohusu fukwe zetu na mazingira kwa ujumla zimenipa matumaini"amesema Dkt. Mpango
Katika hotuba yake Dkt.Mpango ametoa maelekezo kwa wakuu wa Mikoa wote kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuweka mikakati endelevu kwenye fukwe zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo kutatua changamoto zote zinazorudisha nyuma uendekezwaji wake.
"Hapa niseme ukweli bado sijaridhishwa Mikoa kama Dar-es-a-Salaam,Tanga,Lindi,Mwanza na Zanzibar bado inakabiliwa na changamoto ya kuendeleza fukwe zake,utumiaji wa shughuli nyingi zisizo stahili kandoni mwa fukwe zetu umeshamiri ukiwemo uvuvi haramu wa kutumia baruti,sasa mpo hapa wataalamu muone muarobaini wa kulimaliza tatizo hili"amesisitiza Makamu wa Rais Mhe.Mpango.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye leo amekaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Meja Generali Suleiman Mzee amesema Mkoa huo una jumla ya fukwe 31 ambapo mwaka 2021-22 zilitembelewa na watu 11,280 na 2022-23 walitembelea zaidi ya watu elfu tano
"Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuyafanyia kazi maelekezo yako Mhe.Makamu wa Rais ikiwemo usimamizi wa mazingira hasa suala la ukataji miti ovyo ili iwe vyanzo imara vya maji"Mhe.Merry Masanja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Akizungumzia faida za fukwe Prof.Ally Makaya ametokea mfano nchi ya Afrika Kusini imekuwa ikipata faida kila mwaka kutokana na uwekezaji wake ktk eneo hilo ikijikusanyia Randi bilioni 9.3.
Kongamano hilo linalofanyika kila mwaka limebeba kauli mbiu ya Usimamizi madhubuti wa Fukwe kwa Maendeleo nchini Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.