Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima amewakumbusha Makandasi nchini kufanya kazi zao kwa weledi,ubora na kumaliza kazi kwa wakati ili kujijengea kuaminiwa na Serikali na kupewa Miradi zaidi.
Akifunga kikao cha mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Makandarasi CRB na Wadau wa Sekta ya ujenzi leo Jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Katibu Tawala Mkoani humo Bw.Balandya Elikana amesema bado baadhi ya Makandarasi wanafanya ubabaishaji wa miradi wanayopewa na Serikali na kusababisha kuzorotesha kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Yalikuwepo malalamiko mengi siku za nyuma kutoka kwa Makandarasi wazawa kukosa Zabuni mbalimbali za miradi ya Serikali na hii ilitokana na ukosefu wa weledi lakini sasa hali imekuwa nzuri ila tuongeze juhudi".Amesisitiza mtendaji huyo wa Mkoa.
Amesema ana imani Mkutano huo wa siku mbili wa kujengeana uwezo kwa Makandarasi wa ndani kutoka kanda ya ziwa utakuja na matokeo chanya kwa manufaa ya Taifa letu
Ameongeza kuwa maazimio yote kumi waliyoafikiana kwenye mkutano huo Serikali itayapokea na kuyafanyia kazi kulingana na wakati na uzito wa jambo husika likiwemo suala la kupunguziwa kodi kwa vifaa vinavyoagizwa,CRB iwachukulie hatua kali Makandarasi wanaokwenda kinyume lakini kwa kuzingatia mujibu wa Sheria.
Amewakumbusha pia Mkoa wa Mwanza upo eneo la kitovu cha biashara una miradi mingi ya kimkakati inayoendelea kufanyiwa kazi na mingine itakuja hivyo Makandarasi wana wajibu wa kufanya kazi zao kwa usahihi ili kupata Zabuni hizo.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Rhoben Nkori amebainisha
mkutano huo una jumla ya washiriki 320 wakiweno Makandarasi 224 na wadau wengine wanaoshirikiana nao, wamejadiliana changamoto mbalimbali na mikakati ya kuweka mazingira ya kuzidi kupewa zabuni na Serikali.
"Tuna furahi kufanya kazi na Serikali ya awamu ya Sita ambayo ni sikivu na yenye kuwapigania maendeleo watanzania,ni wajibu wetu kukutana kama hivi na kuona wapi tunakosea,nini kifanyike na kuishauri pia Serikali ili kuwepo na tija katika kusukuma guruduma la maendeleo la Taifa letu.Mhandisi Rhoben Nkori.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.