Wadau wa Kilimo na wajasiriamali kwa ujumla katika sekta ya hiyo wameaswa kuyatumia maonesho ya Nanenane mwaka huu Mwanza kuja na matokeo chanya kwa kufanya shughuli zao kisasa zaidi na kuwa na tija.
Akizungumza leo maeneo ya Nyamhongolo mara baada ya kukagua maandalizi ya maonesho hayo yatakayo zinduliwa rasmi kesho,Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu,Ndg. Daniel Machunda aliyemuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza amesema maonesho ya mwaka huu yataambatana na fursa za kuelimishwa namna ya kufanya shughuli kuanzia za Kilimo kwa kisasa zaidi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.
"Nimefarijika kwanza kwa hamasa ya watu kujitokeza kwa wingi,nimejionea shughuli mbalimbali za wadau na hasa Taasisi za kifedha zilizojitokeza kuonesha huduma zao ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania," amesema Machunda.
"Tupo hapa kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu huduma zetu na utambuzi sahihi wa fedha zetu hasa kutokana na ulaghai wa fedha bandia uliopo sasa hivi,wapo wataalamu mbalimbali kwenye banda letu watakao toa ufafanuzi mbalimbali,"Issa Pagali,msimamizi banda la BoT
"Tunashukuru tena kupata fursa hii,Serikali yetu imeweka mkakati mzuri wa mageuzi katika kilimo kuanzia ufugaji wa kisasa na wenye tija,nina mifugo yangu ambayo sasa inanipa faida kutokana na maonesho haya ya Nanenane baada ya kukutana na wataalamu walionielimisha," Elizabeth Masatu,mkulima.
Mratibu wa Maonesho hayo Kanda ya Ziwa
Magharibi,Peter Kasele amebainisha maandalizi yote yamekamilika kuanzia maboresho ya mazingira na usalama kwa muda wote wa Maonesho hayo yatakayo zinduliwa rasmi alhamisi hii na wale walio mbali na Mwanza watayashuhudia mubashara kupitia luninga ya Star Tv.
Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kila mwaka Mwezi Agosti yanaandaliwa kwa kushirikisha Mikoa ya Mwanza kama wenyeji pamoja na Geita na Kagera wanaounda Kanda ya ziwa Magharibi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.