Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amewataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na Sheria za nchi kwa kuiweka jamii kwenye malezi yanayolinda tamaduni na maadili yanayokubalika.
Mhe. Malima ametoa agizo hilo leo Februari 27, 2023 akipokua akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO) Mhe.Mwantumu Mahiza alipofika Mkoani hapo kwa ziara amefanya ziara ya kukagua Mashirika yanayotekeleza Afua za Watoto walio katika mazingira magumu.
Malima amesema mashirika yasiyo ya Kiserikali yana wajibu wa kushirikiana na Serikali kutokomeza ukatili kwa watoto na makundi maalum nchini na kuhakikisha mila za Kitanzania zinalindwa na kukemea matendo yote mabaya kwa jamii.
"Nawashukuru sana kwa kuja kwani hili mnalolifanya ni jambo kubwa katika kukemea maovu nchini kama vile kukomesha watoto wa mtaani na Mungu awasimamie kwani mnaokoa vizazi kwa sasa na baadae kwa kumomonyoka kimaadili kwa majukumu yenu ya kila siku." Mkuu wa Mkoa.
Vilevile, amemuahidi mwenyekiti huyo kuwa Ofisi yake itafanya ukaguzi wa taasisi zote mkoani humo ili kujiridhisha na namna wanavyotekeleza kazi zao na vyanzo vya mapato katika kutimiza wajibu wao kihalali kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.