Mchakato wa Ujenzi Hospitali ya Seko Toure uanze haraka: Naibu Katibu Mkuu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameutaka uongozi wa Mkoa wa Mwanza kuanza mchakato wa ujenzi wa ghorofa tisa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Seko Toure baada ya Serikali kutoa fedha.
Akizungumza leo February 20, 2024 na watumishi wa Hospitali hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa, Mtendaji huyo wa Wizara amesema tayari shs bilioni moja za ujenzi huo zimetangulizwa hivyo hakuna budi kazi ianze.
"Nimeona mpango kazi wote kutoka kwa Mhandisi wa mkoa, naomba sasa tusiwe na sababu zaidi ya kuwaharakishia huduma bora wananchi," amesisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo.
Akitoa taarifa fupi wakati wa mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amesema kutokana na kasi ya ukuaji wa kiuchumi huduma za jamii kama Hospitali ni muhimu sana.
"Ndugu Naibu Katibu Mkuu kwa ukubwa wa Mkoa wetu tunahitaji huduma nyingi na bora za Hospitali, tunashukuru kwa Serilali yetu kutujali na kutoa kipaumbele kwa miradi mingi ya afya hapa mkoani kwetu", Balandya
"Tumepokea kwa awamu fedha za ujenzi Hospitali ya Seko Toure na michoro yote imekamilika tupo mbioni kumpata mkandarasi mshauri ili kazi ianze,"amesema Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Thomas Rutachunzibwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.