Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, amewataka wakazi wa maeneo ya Kigoto na Kabuholo katika Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kuhakikisha wanalinda na kuzuia ujenzi holela unaoendelea katika maeneo yote yenye mgogoro na jeshi la polisi, huku akiwataka kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kushughulikia tatizo hilo.
Mhe. Lukuvi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo yenye mgogoro katika wilaya ya Nyamagana na Ilemela Jijini hapa baada ya kutembelea eneo hilo na kushuhudia nyumba 664 na kaya 461 ambazo zimejengwa Katika eneo hilo lenye mgogoro.
Mhe.Lukuvi ameongeza kuwa, ameona maendeleo makubwa yaliyofanywa na polisi na wananchi hivyo baada ya kuhitimisha ziara yake atashauriana na Mhe. Rais Dk. John Magufuli kuona namna ya kutatua tatizo hilo.
Wakielezea malalamiko yao baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo Wamesema walikuwepo katika maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 40 na wanalipia kodi zote za serikali ikiwemo kodi ya ardhi na majengo na kwa sasa wanaiomba kwa Serikali iwarasimishie maeneo hayo na jeshi la Polisi wabakiziwe eneo lao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.