Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe.Mhandisi Robert Gabriel, amewataka watendaji Mkoani humo kuepukana na vitendo vya rushwa pamoja na kuondoa urasimu ili kuwawezesha wawekezaji kufanya shughuli zao bila tatizo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Biashara kilichofanyika mkoani humo, Mhe.Mhandisi Gabriel amesema wanaohitaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali.
“Wakati mwingine mwekezaji anakuja anakutana na changamoto nyingi, naomba sana watendaji tuwapunguzie mzigo hawa wawekezaji,” alisema Mhe.Mhandisi Gabriel.
Mhe.Mhandisi Gabriel amewahakikishia wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza kuwa ofisi yake itatumia nguvu zote kuhakikisha wanafanikiwa pamoja na usalama wao na mali zao na kuondoa vikwazo vyote vya rushwa.
“Ukiona unazungushwa ni dalili za rushwa na rushwa haitakuwa na mlango katika mkoa huu kwa mwekezaji yeyote,” alisema Mhandisi Gabriel.
Aidha, amesema wanatakiwa kutumia miundombinu kusafirisha malighafi kutoka mkoani humo kwenda sehemu nyingine kwa lengo la kuleta mapinduzi ya kibiashara.
"Hizi barabara siyo za kubeba watu pekee, tunahitaji ndege za mizigo zitue na kesho tujue katika reli ya kisasa ni tani ngapi zitawekwa zipelekwe maeneo mengine,” aliongeza.
Ameongeza kuwa ili uchumi uwe vizuri wanahitaji shehena za mizigo ambazo zinatoka Mwanza kwenda kwenye masoko mengine.
Mhe. Gabriel amemtaka kila mmoja kutumia kanuni, sheria na taratibu kuhakikisha anawajibika kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara.
Naye Dkt. Elibariki Mmari ameziomba halmashauri zote kukaa pamoja na wafanyabaishara ili kupanga tozo ya (service levy).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.