MHE. MARRYPRISCA AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA SIKU MBILI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Januari 13, 2025 ametembelewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi MarryPrisca Mahundi aliyepo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi katika Wilaya za Nyamagana, Sengerema kuanzia tarehe 13 hadi 14, Januari 2025.
Akuzungumza mara baada ya kumpokea Mhe. Mtanda amempongeza Mhandisi Mahundi kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii licha ya kuwa amebadilishiwa Wizara na kuahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano na yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote atakaohitajika.
Naye Mhe. Mhandisi Marryprisca amemshukuru Mhe. Mtanda kwa ukarimu na kumuomba kuendelea kufanya kazi kwa karibu HH na Wizara hiyo hususani kushauri pale anapoona kuna umuhimu wa jambo fulani lenye kujenga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.