Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Albert Chalamila amewataka wananchi wote wa Mwanza na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi wakati wa ziara ya siku tatu ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Mwanza.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Mhe. Chalamila amesema Mhe. Rais Samia atakuwa na ziara kuanzia Juni 13 hadi 15,2021 ambapo ataanza na ufunguzi wa mtambo wa uchenjuaji dhahabu Mwanza na ufunguzi wa jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kanda ya Mwanza.
Mhe.Chalamila ameongeza kuwa Juni 14 atazindua mradi wa maji Misungwi pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR-Fela) Kati ya Mwanza hadi Isaka.
Aidha, Tarehe 15 atatembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kigongo ,Busisi pamoja na kuongea na vijana wote wa Jijini hapa.
"Nawaomba vijana wote wa Mwanza watumie fursa hiyo kwani niyamuhimu kwao, hivyo wajitokeze kwa wingi."Amesema Chalamila.
Hata hivyo amesiaitiza kuwa ziara hiyo ya Mhe.Rais ni muhimu kwani uwepo wake ni faraja kwa wakazi wa Mwanza na mikoa ya jilani hivyo wajitokeze kwa wingi .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.