Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa amewaahidi Wananchi wa Kisiwa cha Irugwa kituo cha afya,boti,kivuko na kuboresha huduma za jamii ,shule za msingi na sekondari.
Alitoa ahadi hiyo leo kwenye Mkutano wa kampeni akiwoambea kura mgombea Urais wa CCM. Mhe.Dkt. John Magufuli, uliofanyika katika Kijiji Cha Nabweko kisiwani Irugwa,wilayani Ukerewe.
Akihutubia umati wa wananchi wa kisiwa hicho, Mhe.Majaliwa amesema hawana budi kuichagua Serikali ya CCM iendelee kuleta maendeleo, kutatua changamoto zao na kuwahudumia kwa dhati.
Alisema wote ni mashahidi kazi za maendeleo zilizofanywa na serikali kwa miaka mitano zinaakisi maisha ya Watanzania wote na ndiyo maana anamwombea kura Mhe.Rais Dkt. Magufuli, amejipanga kuwatumikia kwa kipindi cha miaka mitano mingine ili malengo yaweze kufikiwa.
“ Nchi hii inahataji kupata kiongozi mwenye dhamira ya wazi ya kutunza amani,hayo maendeleo mnayoyaona ni matokeo ya uadilifu wa ukusanyaji wa kodi na kuisimamia ili itumike kupunguza matatizo ya wananchi,kazi iliyofanywa kwa uadilifu na Dkt. Magufuli,”alisema Mhe. Majaliwa.
Alisema kuwa kisiwa cha Irungwa na wilaya ya Ukerewe ya changamoto ya huduma za afya, hivyo baada ya uchaguzi na Rais akishaapishwa atahakikisha kituo cha kwanza cha afya kujengwa Ukerewe ni Irungwa ili kuwasogezea huduma, kuwaondolea wananchi adha ya kuzifuata jijini Mwanza.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema kwa ukubwa wa kata ya Irugwa kinahitajika kituo cha afya ili wagonjwa wenye matatizo ya kiafya wapate huduma karibu, nje ya hapo ni gharama na watu kupoteza maisha.
“Nataka niwambie, tumejenga zahanati 1,498 vijijini na vituo cha afya 498 nchi nzima hapa Ukerewe vitatu (Muriti, Kagunguli kwa zaidi ya sh. bilioni 1,ili kuwapunguzia umbali na gharama za usafiri na kutumia mitumbwi kufuata huduma, Mkundi aje kuchukua fedha za vituo vya Ukerewe na cha kwanza kujengwa ni Irugwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.