Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewataka wanafunzi Kujituma, kuweka bidii ya kizalendo na kufuata Sheria na Taratibu za Michezo ili kupata wanamichezo bora watakaouwakilisha Mkoa kwenye michezo ya UMITASHUMTA Kitaifa Mkoani Tabora mwishoni mwa mwezi.
Ametoa wito huo leo Julai 19, 2022 wakati akifungua Michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) inayowakutanisha wanafunzi 660 kutoka Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki michezo hiyo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nsumba.
"Wachezaji mliochaguliwa kushiriki michuano ya Mkoa mnapaswa kujituma ili muweze kufuzu michuano ya Mkoa, Kitaifa na hata badae ya kimataifa kwani vipaji ni ajira na biashara hivyo zingatieni yote ili mtimize ndoto zenu." Amesema.
Martin Nkwabi, Afisa Elimu Mkoa amesema kuwa kwenye mfumo wa Elimu kuna uhusiano mkubwa sana kati ya elimu na michezo na ndio maana sehemu ambayo michezo imeimarika watoto wanafaulu zaidi kwakua afya ya mwili inafungua akili vizuri zaidi.
Amefafanua kuwa michezo husaidia kufuta ubaguzi wa makabila, elimu, rangi na kufanya watu kuwa wamoja na wenye mshikamano kwani kinachozingatiwa ni umahiri tu uwanjani bila kujali ni nani ameonesha kipaji hicho.
Joseph Mambo, Mratibu wa UMITASHUMTA Mkoa wa Mwanza 2022 amebainisha kuwa mashindano hayo ngazi ya Mkoa yatadumu kwa siku tano na watakaofuzu watauwakilisha Mkoa Kitaifa Mkoani Tabora mwishoni mwa Mwezi Julai mwaka huu.
Vilevile, amefafanua kuwa mashindano hayo muhimu yatahusisha pia wanafunzi kutoka makundi maalumu yatasaidia kuwaunganisha vijana wa Tanzania kitaifa, kupanua wigo wa ufahamu wa watoto kijiografia na kuibua vipaji na taaluma kwa watoto ni miongoni na taaluma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.