Mahakama kuu Kanda ya Mwanza yafanikiwa kusikiliza mashauri 656 kwa mwaka 2020 kwa njia ya mtandao ikiwa ni mashauri mengi zaidi katika kipindi cha dhoruba la covid 19.
Akizungumza katika kilele cha siku ya sheria Nchini kilichofanyika kwenye viwanja vya Mahakama kuu Kanda ya Mwanza Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Mwanza Mhe.Jaji Sam Rumanyika amesema ukamilishaji wa mashauri hayo umefanikiwa kutokana na ubora wa utendaji kazi wa kila mtumishi.
"Mifumo yote hii imejengwa na kuendeshwa na watumishi wa Mahakama kwa umiliki wa asilimia miamoja"alisema Mhe.Jaji Rumanyika.
Aidha,aliongeza kuwa ili kuhakikisha huduma inawafikia wananchi Mahakama ilianzisha Mahakama inayotembea ambapo kwa Mwanza inatoa huduma kwenye vituo vya Buhongwa,Igoma na Buswelu na kuwataka Halmashauri za Jiji(Nyamagana na Ilemela) kutosita wakati wowote wa kazi kutoa taarifa pale wanapohitaji huduma hii maalum hasa kwenye mashauri ya operesheni za uvuvi na uwindaji haramu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Dkt.Severine Lalika akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema Tekinolojia ya TEHAMA imerahisisha utendaji wa Mahakama.
" Mifumo ya Mitandao ya Mahakama imeboresha huduma za upatikanaji wa Nakala za hukumu na malipo ya ada za mashauri mbalimbali,"alisema Dkt.Lalika.
Naye,Mhe.Jackson Bulashi Mwanasheria wa Serikali akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof.Adelardus Kilangi amesema Serikali ilitambua kuwa mifumo ya utoaji hali tuliyorithi kutoka kwa wakoloni haikuweza kuendana na kasi ya maendeleo ya jamii huru ya Kitanzania kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.
"Hii ilipelekea Serikali kuteua kamisheni maalumu ambayo ilijikita katika maboresho ya mfumo wa mahakama,"alisema Mhe.Bulashi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.