Mwenge wa Uhuru leo Agosti 27, 2025 umezindua Zahanati katika kijiji cha Nyashimba wilayani Magu iliyojengwa kwa Tshs. Milioni 92.2 kutoka chanzo cha makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza kuipokea zahanati hiyo, Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa 2025 Bw. Ismail Ali Ussi amewapongeza Viongozi wa Halmashauri na Wilaya hiyo kwa kutoa fedha ambapo amesema zitasaidia kuboresha huduma hususani za mama na mtoto na kupelekea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Aidha, amewapongeza wananchi kwa kuchangia nguvu kazi kwa zaidi ya Tshs. Milioni 16 kwani wameonesha uzalendo na kiu ya kupata huduma bora za afya jirani na makazi yao na kupelekea kuukwamua mradi huo uliochelewa tangu mwezi Januari, 2018 hadi ilipokamilika mwezi Agosti, 2025.
Aidha, Mwenge wa uhuru umeleta neema kwa wananchi wa kijiji cha Njicha-Ihayabuyaga kwa kuwazindulia mradi wa maji uliogharimu zaidi ya Milioni 256 zilizotolewa na Shirika la Lotary Club (SLC) unaozalisha lita elfu 5 kwa saa ambao umeinua hali ya upatikanaji wa maji safi kutoka 37% hadi 74 kwa wakazi wa eneo hilo.
Akizindua mradi huo, Kiongozi wa mbio za Mwenge amewapongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kujenga mradi huo na kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya faida ya mradi na kupelekea kutoa eneo la ujenzi bure pamoja na kuchangia nguvu kazi.
Mradi huo wa maji unahudumia wananchi zaidi ya 4500 ambao ni sawa na asilimia 75 ya wakazi wote katika kijiji hicho ambao una miundombinu kama visima 2, matenki 6, minara 2, mtandao wa bomba pamoja na sehemu za kuchotea maji.
Mradi wa vijana waosha magazi waliokopeshwa milioni 30 na halmashauri umefungua dimba kwa mbio za mwenge wa uhuru wilayani humo kabla ya kukagua miundombinu ya Nishati Safi ya kupikia katika shule ya sekondari ya wasichana yenye thamani ya Milioni 13 na kuhitimisha kwa kuzindua barabara ya RC Hostel mjini Magu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.