Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike amesema Ofisi yake itaongeza nguvu ya wataalamu wake kwenye miradi inayotekelezwa Wilayani Sengerema ili kuongeza kasi ya ukamilishwaji ili Wananchi wapate huduma zote za msingi,Mtendaji huyo wa Mkoa amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayofanywa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI,Dkt. Switbert Mkama Mkoani Mwanza.
"Wananchi wetu hawana sababu ya kukaa muda mrefu kusubiri Maendeleo,ni wajibu wetu kuwaharakishia Maendeleo" kauli ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike wakati wa ukaguzi wa Miradi mbalimbali Wilayani Sengerema akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt Switbert Mkama.
Kwa upande wake Dkt Mkama amewahimiza viongozi wa Halmashauri ya Sengerema kuhakikisha miradl yote wanayoitekeleza iendane na thamani ya fedha.
Miradi inayotekelezwa Wilayani humo ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari,Hospitali pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya Sengerema
Naibu Katibu Mkuu Dkt Mkama yupo Mkoani Mwanza kwa ajili ya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa Mkoani humo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.