• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MIRADI YA ELIMU MSINGI IKAMILIKE KABLA YA FEBRUARI 28 - RC MTANDA

Posted on: February 9th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameagiza kwamba miradi yote inayotekelezwa katika sekta ya elimu msingi, iwe imekamilika ifikapo Machi 28, 2026.

Agizo hilo amelitoa leo Februari 09, 2025 alipokuwa akikagua ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya Bukanda, iliyopo Kata ya Bukanda, Wilaya ya Ukerewe.

Mhe. Mtanda amesema kuwa serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika Wilaya ya Ukerewe, ambapo miradi hiyo inaendelea kutekelezwa katika sehemu mbalimbali za wilaya hiyo.

“Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya elimu msingi, na ni muhimu miradi hii ikamilike kwa wakati ili wananchi wa maeneo haya wafaidike na huduma bora za elimu,” amesema Mhe. Mtanda.

Ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha utekelezaji wa miradi hii unakamilika kama ilivyopangwa, akiwataka Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata, na Watendaji wa Vijiji kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unafanikiwa.

Aidha, Mhe. Mtanda ameeleza kuwa serikali pia imetoa shilingi milioni 201 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu sekondari katika Wilaya hiyo, ambapo amesisitiza kuwa usimamizi wa miradi hiyo inapaswa kuwa wa kiwango cha juu.

“Hatutaki kuona miradi hii ikiishia nusu. Tutasimamia kwa karibu na nitaita mkutano mkoani kujadili na kutathmini utekelezaji wa miradi hii. Hakuna kubweteka,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtanda ametoa pongezi kwa wananchi wa Wilaya ya Ukerewe kwa kuitikia wito wa uandikishaji wanafunzi, akibainisha kuwa kiwango cha uandikishaji kimepanda kwa kiasi kikubwa. Kwa Darasa la Awali, kiwango cha uandikishaji kimefikia 105%, Darasa la Kwanza 94%, na Kidato cha Kwanza 85%.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI IDARA YA MAAFA OWM AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA DHARULA MWANZA

    February 20, 2026
  • KAYA 19,344 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE MWANZA AWAMU YA KWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.