MIRADI YA MAJI YA ZAIDI YA SHS BILIONI 34 YATEKELEZWA SENGEREMA:DC NGAGA
Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imepewa pongezi kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maji wilayani Sengerema yenye thamani ya zaidi ya shs bilioni 34 ambayo imeongeza kasi ya maendeleo
Miradi hiyo inayotekelezwa na Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini,RUWASA imenufaisha vijiji vingi wilayani humo vikiwemo Chimfumfu,Nyakahabo na Lukumbi ambapo jumla ya wananchi 31000 kutoka vijiji hivyo wamenufaika.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga ametoa taarifa hiyo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza,Balandya Elikana alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wa Kijiji cha Chimfumfu kuona wanavyo nufaika na miradi ya maji.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema upatikanaji wa maji vijijini umechangia pia pato la kila familia kutokana na mama kuwa na nafasi ya kufanya shughuli za kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi kusaka maji ya umbali mrefu.
"Tuna ishukuru Serikali kwa kutupatia huduma ya maji safi na salama,sisi wakazi wa kijiji cha Chimfumfu tumefaidika na mradi wetu wa maji,'Bi.Consolatha Medadi,mkazi wa Chimfumfu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Sengerema Mhandisi Francis Masawe amesema mradi wa maji wa Chimfumfu umegharimu shs bilioni 2.9 na kuendelea kuwa na tija kwenye vijiji vitatu.
Aidha Ndugu Balandya amewataka wananchi hao kusimamia na kuilinda miundombinu hiyo ya maji kwa faida ya vizazi vijavyo,kwani Serikali imetoka fedha nyingi ili kuhakikisha wanapata huduma endelevu ya rasilimali hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.