Afisa Biashara wa Mkoa Yesaya Sikindene ameongoza kikao Kazi cha pili cha Maafisa Biashara Mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika Halmashauri ya Buchosa, ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili vyanzo vyote vya mapato vilivyo chini ya kitengo cha biashara na kujadiliana njia na mbinu mbalimbali za kuongeza mapato katika Halmashauri za Mkoa wa Mwanza.
Akiongea katika Kiakao hicho Afisa Biashara wa Mkoa Yesaya Sikindene amesema Vitengo vya biashara katika Halmashauri za Mkoa wa Mwanza hukusanya mapato mbalimbali yatokanayo na ada za Leseni za biashara, ushuru wa Hoteli, leseni za vileo, Vizimba na masoko, pikipiki na bajaji pamoja na adhabu na faini ambazo hutozwa kwa wafanyabiashara wanaokiuka sheria ya leseni za biashara kwa mujibu wa sheria Na. 25 ya Mwaka 1972 pamoja na marekebisho yake.
Kwa Mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya bajeti ya vitengo vya biashara katika Halmashauri zote ilikuwa bilioni 6.6 (6,614,426,793) na hali halisi ya makusanyo ilikuwa bilioni 5.8 (5,844,512,307) sawa na Asilimia 88 ya makisio ya bajeti.
Katika Makusanyo hayo, Halmashauri iliyoongoza kwa kukusanya zaidi ya Bajeti ni Buchosa 146%, Ilemela 115%, Jiji 85%, Misungwi 83%, Ukerewe 78%, Kwimba 69%, Magu 61% na Halmashauri ya Sengerema ilikusanya 48% ya bajeti.
Sikindene ameongeza kuwa Sekta ya Biashara imekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na Upungufu mkubwa wa Maafisa Biashara, Mkoa unapaswa kuwa na Maafisa 56 kwa mujibu wa Ikama waliopo ni 26 tu. Upungufu uliopo ni sawa na 55%.
Vitendea kazi pia ni changamoto kubwa hasa Kompyuta, Printer, Shajala, Meza na viti pia Kukosa magari kwa ajili ya kuendesha operesheni mbalimbali mitaani/vijijini inapelekea kudorora kwa makusanyo,Urasimu na ushirikiano duni baina ya Maafisa biashara na wamiliki wa Viwanda hasa wanapotakiwa kutoa taarifa za Kila robo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.