MKONO WA EID WA RAIS SAMIA WAGUSA WENYE UHITAJI MWANZA
Katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al- Fitri na kutamatika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Eid kwa kambi ya wazee wasiojiweza na vituo viwili vya watoto yatima mkoani Mwanza.
Akiwasilisha zawadi hizo katika kambi ya wazee Bukumbi- Misungwi, Markazi ya watoto yatima ya Sharif Said Nyegezi- Nyamagana pamoja na kituo cha palezi ya watoto cha Kamanga, mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amesema Rais Samia anaendeleza utamaduni wake wa kuwakumbuka wenye uhitaji hivyo ametoa zawadi ili kusherehekea vyema sikukuu pamoja nao
“Wanasema kinywa cha Mzee kina busara sana msiache kumuombea Rais wetu awe na afya njema ya akili ya mwili ili aweze kuliongoza vyema Taifa letu”. Amesema Mhe. Mtanda.
Aidha, Mkuu wa Mkoa akiwa katika kituo cha Markazi ya Sharif Said ameahidi kuchangia kujenga darasa moja ili watoto hao waendelee kupata elimu ya dini itakayowasaidia kuitetea na kuisambaza dini.
Baadhi ya viongozi kutoka kwenye kambi ya kulelea wazee hao wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuwa na moyo wa kutoa na kulikumbuka kundi hilo ambalo nalo linatakiwa kufurahia sikukuu hizi.
Nao watoto kutoka kituo cha Markazi ya watoto yatima ya Sharif Said Nyegezi wamemshukuru Rais Samia shukrani zilizoambatana na dua maalumu ya kumuombea afya njema na umri mrefu wenye manufaa.
Jumla ya fedha zilizotolewa katika Mkoa wa Mwanza ni shilingi milioni 10 ambapo wamenunuliwa jumla ya mbuzi 12, mchele gunia 12, mafuta ndoo kubwa 12, sukari mifuko 12 na soda katoni 90.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.