Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima ameziagiza Halmashauri na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kushirikiana kupeleka Maji safi na salama kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya pamoja na taasisi za Elimu mkoani humo ili kupunguza adha kwa watumishi na wananchi wanaopata huduma.
Akikaguzi Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Buzilasoga wilayani Sengerema unaotarajia kuwahudumia zaidi ya wananchi 1852 chini ya Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF III) kwa zaidi ya Milioni 543, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema huduma za Afya haziwezi kutolewa pasipo kuwa na Maji ya kutosha.
Amesema pamoja na fedha za Mradi huo kuhusisha Ujenzi wa Miundombinu kama vile Wodi ya Wazazi, Watoto, Maabara na Jengo la Kupokelea wagonjwa wa nje ni lazima Halmashauri na RUWASA kushirikiana kutafuta fedha za kuchimba kisima kirefu cha maji mara moja kabla ya kuanza kwa kutoa huduma.
"Kituo cha Afya bila huduma za Maji haiwezekani na tusidanganyane na kutegemea chanzo cha maji ya mvua badala yake naomba Halmashauri itenge angalau Milioni 30 hapa ili tupate kisima kirefu cha maji kwenye kituo hiki." Amesema Malima.
Aidha, ameagiza Halmashauri hiyo kuongeza muda wa kufanya kazi na Rasilimaliwatu ili hadi kufikia Machi 15, 2023 mradi huo uwe umekamilika na ili kuweza kutimiza vigezo vya kuendelea kupata ufadhili wa miradi mingine ya maendeleo.
Naye, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana amewataka wananchi wa kijiji cha Mami kilichopo kata ya Kishinda kuendelea kujitolea nguvu kazi kwenye mradi ya Maji wa Zahanati ya Kijiji ambapo Mkuu wa Mkoa amechangia Shilingi Laki 5 kuunga mkono juhudi za wanamchi wanaochimba mtaro wa Maji.
"Mhe. Mkuu wa Mkuu, Mradi huu umefikia Asilimia 80 ya Ujenzi na tunatarajia kuukamilisha baada ya wiki moja" Amesema Ndugu. Malisa Nguda, Mratibu wa TASAF Wilaya ya Sengerema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.