Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ametoa siku saba kurejeshwa mifuko 263 ya saruji iliyoibiwa wakati wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto lenye usanifu wa sakafu sita unaoendelea katika hospital ya rufani ya Sekou-Toure.
Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwepo kwa taarifa ya kuibiwa mifuko hiyo ambayo inakwamisha ukamilishaji wa ujenzi huo kwa wakati huku baadhi ya walinzi wa wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Hivyo alimtaka OCD Mkoa kufatilia kwa undani suala hilo ili wahusika wakamatwe huku wakiacha uonevu wa kuwakamata walinzi ambao yawezekana hawakuhusika bali wanabambikiziwa kesi kwa sababu ni watu dhaifu hivyo uchunguzi ufanyike wakibainika ni wao wachukuliwe hatua.
"Hata kama ni Mkuu wa Mkoa au kiongozi yeyote amehusika akamatwe asiogopwe na kupewa kesi watu wengine ambao ukiangalia ni watu wanaotafuta ridhiki tu " alieleza Mongella .
Aidha Mongella hakurizishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo hivyo aliwagiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)kuongeza juhudi ,kujenga kwa ubora kwa kuweka vifaa vilivyokidhi viwango na kukamilisha ujenzi huo .
Kwa upande wake Moses Urio Kaimu Meneja wa TBA alisema mradi huo upo katika hatua ya ukamilishaji wa kazi ikiwemo upigaji wa skimming,rangi nje ya jengo ,uufitishaji wa madirisha na uwekaji wa terazo hadi sasa unefikia asilimia 80 ya Kazi zote.
Alisema mradi huo utakapokamilika utaboresha huduma ya afya kwa wananchi hususani akina mama na watoto ,utapunguza msongamano kwa wagonjwa uliopo sasa ambapo utatoa huduma kwa vitanda 261 na utapunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.