Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameanza ziara yake ya kikazi ya siku nne Wilaya ya Ukerewe na kupokea taarifa ya afya katika zahanati ya Sizu iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dtk.Raphael Mhana.
Dkt.Raphael amesema kuwa zahanati ya Sizu imejipanga kuhakikisha inapunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuhamasisha kujifungulia kituo cha afya,pia kuwapa elimu ya kuhudhuria kliniki.
Aidha Tabibu Msaidizi Elizabeth John amesema kuwa wana changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufinyu wa jengo la kutolea huduma,kutokuwa na chanzo cha uhakika cha umeme na baadhi ya wakina mama kutokujifungulia kituoni na kutokuwa na usafiri wa uhakika kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa wa dharula.
"Zahanati ya Sizu ina watumishi wawili tu tofauti na mwaka jana ilikuwa na watumishi watatu,tunaendelea kuomba mamlaka husika ili kutuongezea watumishi, aliaema Elizabeth.
Akipokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amehoji matumizi ya dawa kwani amekuta hakuna bini kadi na amerekodi wagonjwa 25.
"Inakuwaje kati ya wagonjwa 300 unarekodi 25 pekee na dawa zinaonekana kutumika unafanyaje kuomba dawa nyingine pindi zinapoisha au unabuni kichwani tu,alihoji Mongella.
Mhe.Mongella akihutubia wananchi katika viwanja vya Shule ya Msingi Sizu amesema kuwa kwenye maendeleo lazima tujitoe ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anashiriki.
Hata hivyo Mhe.Mongella amechangia shilingi laki moja kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya Msingi Sizu na wataka kila mmoja kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Mhe.Mongella amekemea unyanyasaji na uvuvi haramu na kuongeza kuwa visiwani kusiwe sehemu ya uovu,ualifu na uvunjifu wa Sheria na kuwataka kila mmoja kuwa mlizi wa rasilimali za kijiji.
"Wote tuungane katika kutumia rasilimali zetu ili vizazi vijavyo binufaike na rasilimali hizi,alisema mongella."
Naye Mwekekiti wa Halmashauri George Nyamaha amesema kuwa tokea Nchi hii ipate uhuru 1961 ni mara ya kwanza kwa Mhe.Mkiu wa Mkoa kutembelea kisiwa cha Sizu kata ya Kagunguli iliyopo Kijiji cha Sizu.Kisiwa cha Sizu kina wakazi 6406 kwa takwimu ya 2020 na ilianzishwa mwaka 1971.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.