Mshindi wa jumla wa mashindano ya kwaya katika tamasha la Urithi wetu (Urithi Festival) Kwaya ya Mt. Benedikto ya Bugando Mkoani Mwanza wakabidhiwa zawadi ya gari aina Toyota Nissan Suzuri maarufu kama kirikuu yenye thamani ya million 30.
Aidha kwaya zilizoingia kwenye mchakato zilikuwa 26 na baada ya mchujo ulioendelea zilibaki kwaya tisa zilizofika kwenye kilele jijini Mwanza na kwaya ya Mt.benedikto kuibuka kidedea.
Aliongeza kuwa katika warsha hiyo mshindi wa kwanza alijinyakulia zawadi ya gari, mshindi wa pili ambaye ni kwaya ya Mt.Aloyce Gonzaga akiondoka na zawadi ya pikipiki huku mshindi wa tatu kwaya ya Mt.Yohana Mwinjili wakipata vyombo vya mziki.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala, alisema lengo la kuanzishwa kwa tamasha hilo lililiofanyika Oktoba 31 hadi Novemba 3 mwaka jana jijini Mwanza,ambapo kwaya hiyo iliibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo yenye lengo la kutambua thamani ya urithi wa mtanzania vikiwemo vyakula mila na desturi .
Alisema tamasha hilo lilianza mwaka 2018 ambapo litakuwa linafanyika kila mwaka, litasaidia kudumisha na kukumbusha utamaduni,mila,desturi na kuhamasisha uzalendo wa nchi,hivyo aliwahimiza watanzania hususani waimbaji kuhamasisha jamii kwa kutumia nyimbo ili itambue uzalendo na kuelewa uhalisia wao na mali ambazo ni urithi wa taifa.
“Naishukuru Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro kwa kutimiza ahadi ya Serikali ya kutoa zawadi kwa mshindi wa jumla wa mashindano ya kwaya katika tamasha la urithi wetu lililofanyika jijini hapa,”alisema Dkt. Kigwangala.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda,alisema maelekezo ya ushiriki wa kwaya katika tamasha hilo yalitolewa na kuwataka kuandaa nyimbo tatu ambazo ni wimbo wa taifa ambao ni Tanzania nchi yangu nakupenda, wimbo unaohusu utalii na wimbo wowote ambao kwaya itapenda.
Pia alitoa ombi lake kwa Wizara kuwapa nafasi ya upendeleo wakutembelea mbuga za utalii wajionee kwa macho na wasiishie katika kuimba na kuwakumbuka pindi wanapoandaa matamasha mengine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.